The House of Favourite Newspapers

Bilionea Ashusha Neema Tena Yanga

KAMPUNI ya GSM iliyo chini ya Mkurugenzi, Gharib Mohamed, juzi imeshusha mzigo mpya wa jezi za Yanga nchini baada ya ule wa awali kumalizika saa chache mara baada ya kuzinduliwa. GSM hivi karibuni ilishinda zabuni ya kutengeneza jezi za Yanga za msimu huu kwa shilingi bilioni 1.3 kwa kipindi cha miaka mitatu.

 

Akizungumza na Championi Jumatano, Kaimu Katibu wa Yanga, Dismas Ten alisema kuwa mzigo huo mpya wa jezi unapatikana kwenye maduka yote ya GSM ya Pugu na Msasani.

 

Ten alisema kuwa, ni nafasi pekee ya mashabiki wa Yanga
kujitokeza kwa wingi kununua jezi hizo tayari kwa ajili ya kwenda kuisapoti itakapokuwa uwanjani Jumamosi hii ikicheza na Township Rollers ya Botswana.

 

“Nichukue nafasi hii kuwatangazia mashabiki wa Yanga kuwa jezi mpya za timu yao, tayari zipo madukani zitakazopatikana kwenye GSM Mall zote za hapa jijini Dar es Salaam,” alisema Ten.

Comments are closed.