The House of Favourite Newspapers

BARNABA ATAJA MANENO YA RUGE AMBAYO HATOYASAHAU

Msanii Barnabas Elias, maarufu kama Barnana Classic leo amefanya ziara ya utambulisho wa nyimbo yake mpya inayoitwa ‘ Isweke ‘ ndani ya studio za + 255 Global Radio zilizopo Sinza Mori, Dar es salaam. Akifanya mahojiano maalumu na kipindi cha Bongo 255 kinachoruka hewani kila siku kuanzia saa Sita mpaka saa kumi jioni, Barnaba ameongelea mambo mengi kuhusu maisha, muziki na mipango yake ya siku za usoni.

Akizungumzia kuhusu mafanikio yake ya kimuziki, Barnaba amesema kuwa anajivunia kwa hatua aliyofikia kwani ni hatua kubwa, na anamshukuru sana Mungu pamoja na Marehemu Ruge Mutahaba kwa kumuonyesha njia. Zaidi ya hapo amesema anajivunia kuwa na mchango katika mafanikio ya baadhi ya wasanii wakubwa hapa nchini katika ‘angle’ ya uandishi, kwani amewaandikia nyimbo nyingi sana wasanii wakubwa Tanzania kama vile Shilole, Nandy, Lulu Diva, Linah, Mwasiti, Recho, Ruby  na wengine wengi, nyimbo ambazo zimefanya vizuri sana kwenye ‘game’ ya muziki.

” Nilipofungua studio nilimualika Marehemu Ruge kuja kuiona, alifurahi sana na kuniambia maneno haya ambayo sitakaa niyasahau. Aliniambia kuwa ‘tumia hii studio kama mwamvuli wa kutengeneza kina Barnaba wengine’ …”

Amefunguka Barnaba Classic na kueleza kuwa ameamua kusajili kampuni yake BASATA na BRELA ili kutimiza kazi aliyoambiwa na Ruge, ya kusaidia wasanii wengine kusimama kimuziki.

Akizungumzia mchango wa BASATA katika tasnia ya muziki, Barnaba amesema BASATA wamekuwa na mchango mkubwa sana kwenye tasnia ya muziki, ila wasanii wamekuwa hawaipi ushirikiano. Akaenda mbali zaidi zaidi na kusema BASATA wana hadi instagram page, lakini wasanii wamegoma hata kuifollow ile page, amewaomba wasanii kushirikiana na BASATA kwani yeye binafsi ameona matunda ya BASATA katika kazi zake.

 

Comments are closed.