The House of Favourite Newspapers

Bill Cosby Afungwa Miaka 10 kwa Unyanyasaji Kingono

Mahakama ya Pennsylvania nchini Marekani imemshushia mvua ya kifungo cha kati ya miaka mitatu hadi kumi, mchekeshaji Bill Cosby mwenye umri wa mika 81, baada ya kumkuta na hatia ya kufanya unyanyasaji wa kingono na ubakaji dhidi ya msichana, miaka 14 iliyopita.

Jaji wa mahakama hiyo amesema Cosby amekutwa na hatia katika makosa matatu aliyoyafanya mwaka 2004, akimnyanyasa kingono na kumbaka msichana aliyetajwa kwa jina la Andrea Constand. Mahakama pia imeamuru Cosby kusajiliwa kwenye orodha ya wanyanyasaji wa kingono na kwamba anapaswa kuhudhuria programu maalum ya kisaikolojia kwa kipindi cha maisha yake yote.

Kwa mujibu wa hukumu iliyosomwa mahakamani hapo, Cosby alimualika msichana huyo nyumbani kwake, kisha akamuwekea vidonge vya dawa za kulevya kwenye kinywaji chake kabla ya kuanza kumuingilia kwanza kwa kutumia vidole vyake. Msichana Andrea Constand, alieleza kuwa kitendo hicho kilimtoa usichana wake, kumsababishia maumivu makali pamoja na matatizo makubwa ya kisaikolojia.

Comments are closed.