The House of Favourite Newspapers

CHILDISH GAMBINO AUMIA MGUU, AAHIRISHA SHOO ZAKE

Image result for childish gambinoChildish Gambino, nimwimbaji, mwigizaji na mchekeshaji maarufu nchini Marekani, ameumia mguu na hivyo kuahirisha ziara yake aliyokuwa aifanye Leo katika kituo cha burudani cha The Forum cha Inglewood, California.

Msanii huyo pia hakufanya shoo aliyopanga Jumapili iliyopita jijini Dallas, ambapo alionekana kwenye baskeli maalum ya wagonjwa na mguu ukiwa umefungwa bandeji.

Habari ya kuumia kwa msanii huyo ni mbaya kwa mashabiki wake ambapo pia alikuwa ameahidi kwamba ziara yake hiyo ya This is America ingekuwa ya mwisho kwa nyota huyo ambaye jina lake halisi ni Donald Grover.

Haijulikani iwapo ataendelea na ziara hiyo ambayo inajumuisha shoo nane.

Comments are closed.