The House of Favourite Newspapers

BILL COSBY KUFUNGWA PAMOJA NA WAFUNGWA WENGINE

Bill Cosby akiwa amevaa nguo za jela.

BAADA ya kutiwa hatiani na mahakama jana kwa unyanyasaji wa kijinsia dhidi ya msichana kwa makosa aliyoyafanya miaka minne iliyiopita, mchekesaji maarufu wa Marekani, Bill Cosby, atafungwa kama wafungwa wengine, labda kama atakuwa na tatizo la kiafya la kulazimu kutochanganywa na wafungwa wengine.

Mchekezaji huyo aliyewahi kujizolea sifa na fedha kubwa kama mwigizaji aliyekuwa analipwa mkwanja mkubwa zaidi duniani miaka ya 1986 na 1987, amehukumiwa kwenda jela miaka mitatu hadi kumi kwa kosa la kumlewesha na kumwingilia msichana huyo.

Hata hivyo, walinzi wa gereza husika wanasema Cosby anaweza akapata kazi yoyote ndani ya gereza hilo hata kama ni utapeli wa kuchekesha.

Image result for bill cosby

 

Comments are closed.