The House of Favourite Newspapers

Zahera Ashusha Presha Yanga

Wachezaji wa Yanga.

KOCHA Mkuu wa Yanga, Mkongo, Mwinyi Zahera amefunguka kuwa hana hofu ya mechi yao na Simba ambayo ndiyo ina mashabiki wengi nchini sababu tayari amefanya kazi na timu zenye mashabiki wengi uwanjani zaidi ya 120,000.

 

Simba na Yanga zinatarajiwa kuvaana siku ya Jumapili ka­tika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam na uwanja huo unabeba idadi ya watu 60,000.

Mwinyi Zahera

Akizungumza na Championi Jumatano, kocha huyo alisema kuwa hana presha kuhusu mashabiki sababu alishawahi kusi­mamia michezo yenye mashabiki wengi zaidi wanaotosha Uwanja wa Taifa.

 

“Kwangu ni furaha kuweza kuiongoza timu yangu kwa mara ya kwanza kwenye mchezo mkubwa kwa hapa Tanzania lakini sina hofu wala presha sababu nina uzoefu kusimamia timu ikiwa na mashabiki wengi zaidi ya 120,000 na hapa ni hao 60,000 na najua presha kubwa inatoka kwa mashabiki, hilo kwangu halipo.

 

“Tayari nimefundis­ha timu tofauti ambazo zina mashabiki wengi huko kwetu Congo hata nikiwa na timu ya Taifa ya DR Congo pale Kinshasa na hii huenda ikawa mechi ya nne ambayo itakuwa na mashabiki wengi kama watajitokeza lakini bado wingi wao kwangu siyo tatizo, zaidi ni kupambana,” alisema Zahera.

BEN POL X CEDO – NTALA NAWE (OFFICIAL VIDEO)

Comments are closed.