Billnass afungukia kupewa gari na Nandy

DAR ES SALAAM: MSANII wa muziki wa Hip Hop Bongo, William Lyimo ‘Billnass’ ameibuka na kufungukia madai yanayosambaa mtandaoni kuwa amepewa gari na aliyekuwa mpenzi wake, Faustina Charles Mfinanga ‘Nandy’ kwa kusema hakuna ukweli wowote juu ya jambo hilo.  Akipinga na Risasi Jumamosi, Billnass alisema ameyaona maneno hayo mitandaoni watu wakidai kuwa Nandy amemnyang’anya gari aina ya Toyota Crown mpiga picha wake na kumpatia yeye kitu ambacho hakina ukweli, yeye anayo magari yake mawili.

“Unajua watu wanapenda sana kuongea ukiangalia gari langu na la yule mpiga picha ni tofauti kabisa, watu wanaongea vitu wasivyovijua,” alisema Billnass.  Aidha, Billnass alisema kuwa yeye anamiliki magari mawili ambayo yote ana kadi zake zinazosoma jina lake. “Mimi ninamiliki magari mawili siwezi kupewa gari na Nandy tena ambalo ameshampa mtu zawadi,” alisema Billnass.

Billnass na Nandy kwa sasa wamekuwa habari ya mjini kufuatia kuachia wimbo mpya unaokwenda kwa jina la Bugana ambao unatikisa kwenye vituo mbalimbali vya redio na mitandao ya kijamii. Wapo wanaodai kuwa Nandy na Billnass wamerejesha mapenzi yao baada ya kuachana kwa muda mrefu lakini Bill mwenyewe amesema kwa sasa wamebaki kuwa marafiki tu!

STORI: MWANDISHI WETU, Risasi Jumamosi


Loading...

Toa comment