Billnass Amfungukia Nandy

MBONA ni washkaji tu! Ndiyo maneno aliyotoa mkali wa Hip Hop Bongo, William Lyimo ‘Billnass’ baada ya madai kusambaa kuwa amerudiana na msanii mwenzake, Faustina Charles ‘Nandy’.

 

Akistorisha na Over Ze Weekend, Billnass alisema, kwa sasa yeye na Nandy wamebaki kuwa washkaji hivyo kuachana kwao hakukuathiri urafiki wao kwa sababu hata kazi wanazofanya zinafanana hivyo mara nyingi huwa pamoja wakisapotiana.

 

“Unajua Nandy ni mshkaji wangu sana, nashindwa hata nikuambie nini, kwa sababu tangu tumeachana tumekuwa marafiki wazuri na yote ni kwa sababu ya kazi tu hakuna kingine, hivyo mara nyingi tumekuwa tukisapotiana,” alisema.

MEMORISE RICHARD

 


Loading...

Toa comment