The House of Favourite Newspapers

Binti Wa Kinigeria Awa Rais Wa Kwanza Mweusi Harvard University

Imelme akiwa na uso wa furaha

Imelme amefuata nyayo za Obama

Ujumbe wa Twitter uliotumwa kwenye akaunti ya Chuo cha Harvard

Habari kubwa inayovuta hisia za wengi mtandaoni hivi sasa, ni kuhusu mwanadada Imelme Umana, 18 kutoka nchini Nigeria ambaye amechaguliwa kuwa mwanamke wa kwanza mweusi kuwa Rais wa Kitengo cha Uchambuzi wa Sheria cha Chuo Kikuu cha Harvard (Harvard Law Review), nchini Marekani.

Imelme anayesomea sheria katika ngazi ya shahada ya uzamili, kabla ya kuteuliwa kushika wadhifa huo, alikuwa mwenyekiti wa kamati ya Huduma kwa Jamii. Urais wa Harvard Law Review ndiyo cheo kikubwa zaidi kwa upande wa serikali ya wanachuo, jambo ambalo linamfanya Imelme kuwa ndiyo mwenye hadhi ya juu zaidi chuoni hapo.

Rais wa Marekani aliyemaliza muda wake, Barack Obama ndiye aliyekuwa mwanaume mweusi wa kwanza kuongoza kitengo hicho, mwaka 1990 kwa hiyo Imelme naye anaingia kwenye historia hiyo, akiwawakilisha wanawake weusi.

Comments are closed.