The House of Favourite Newspapers

Mr. Shinda Nyumba ‘Azama Kitaa’, Akusanya Kuponi Kibao za Droo ya Kwanza

Mr Uwazi (kushoto) akiwa na msomaji wa Kiluvya, Eva na Mr Shinda Nyumba.

Msomaji, Eva Fadhili akijaza kuponi yake.

Mr Shinda Nyumba akimpa zawadi ya sabuni msomaji wa Kiluvya, Abdallah Juma.

Mr Uwazi akitoa maelezo kwa msomaji wa Kibamba, Mwajuma John.

Wadau wa Magazeti ya Global, Bobroy Ngowi na Ally Salumu, wakijaza kuponi zao maeneo ya Kibamba jijini Dar.

Msomaji wa Kiluvya jijini Dar, Renatus Matabi, akijaza kuponi zake.

 

Mr Shinda Nyumba akiwa kwenye pozi na wasomaji.

   Mr Shinda Nyumba – Julius Charles — akigawa vipeperushi vya bahati nasibu ya Shinda

Ofisa Masoko wa Global Publishers, Yohana Mkanda, akizungumza jambo na msomaji wa Kibamba , Sabuni Ally.

ZIKIWA zimebaki siku kadhaa kuelelea Droo ya Kwanza ya Bahati Nasibu ya Shinda Nyumba inayotarajia kufanyika Februari 8, mwaka huu katika Viwanja vya Zakhem- Mbagala jijini Dar, Julius Charles ‘Mr Shinda Nyumba’, amekusanya kuponi za droo hiyo kwa kishindo.

‘Mr Shinda Nyumba’ ambaye anatajwa kuwa ni miongoni mwa watu warefu kuliko wengine nchini ameonekana kuwa kivutio katika viunga mbalimbali vya Jiji la Dar katika zoezi zima la kukusanya kuponi za wasomaji mbalimbali.

Mtu huyo jana alitembelea maeneo ya Kiluvya, Kibamba, Goba na viunga vingine vya jiji ambapo wasomaji walijitokeza kwa wingi kukusanya kuponi zao.

“Wasomaji wanapaswa kushiriki kwa wingi kununua Magazeti ya Kampuni ya Global Publishers ambayo ni Risasi, Ijumaa, Amani, Uwazi, Championi na Ijumaa Wikienda kisha kujaza kuponi iliyopo katika ukurasa wa pili wa kila gazeti.  Nitakuwa napita mara kwa mara kukusanya kuponi pamoja na kutoa zawadi ndogondogo za papo hapo,” alisema Mr Shinda Nyumba.

 

Shinda Nyumba Awamu ya Pili Yatikisa Jiji la Dar es Salaam

Comments are closed.