The House of Favourite Newspapers

Blac Chyna kutoka na mdogo wa Kim Kardashian, Valentine’s Day

0

Black-Chyna-in-Hollywood-SPLBlac Chyna

IMEBAINIKA kuwa mwanamitindo na mcheza utupu, Blac Chyna yupo katika mipango ya kujiachia kimapenzi na mdogo wa mwanamitindo, Kim Kardashian, Rob katika sikukuu ya Valentine’s Day wiki ijayo.

Rob-Kardashian-Blac-Chyna-MainRob na Blac Chyna

Chanzo makini kilianika ubuyu kuwa Blac anayo furaha kubwa kuwa kimapenzi na Rob na kwamba anachotaka siku ya wapenda nao (Valentine’s Day) kuona wakitoka sambamba na ukoo wa Kardashian.

“Anayo furaha kuona wakitoka kama kundi la familia na kwenda kushiriki katika sehemu maalum. Anataka kuwepo na Rob, Kim na Kanye, Kylie na Tyga, Kris na Corey, Khloe na James,” kilisema chanzo.

Blac Chyna awali alikuwa katika mahusiano ya kimapenzi na rapa Tyga na kufanikiwa kuzaa naye mtoto mmoja, King Cairo. Kwa sasa Tyga anatoka na mdogo wa Kim Kardashian, Kylie Jenner.

Imeandaliwa na Andrew Carlos/GPL

Leave A Reply