The House of Favourite Newspapers

Bobi Wine Akamatwa Tena, Apelekwa Kusikojulikana

 

MBUNGE  wa Kyadondo Mashariki, Robert Kyagulanyi, maarufu kama Bobi Wine leo asubuhi amekamatwa na jeshi la polisi nchini Uganda katika kituo cha ukaguzi cha One Love Beach, Busabala.

Wine ambaye pia ni mwanamziki, amekamatwa wakati akitoka Magere maeneo ya Busabala alipokuwa akitarajia kuzungumza na waandishi wa habari kuhusu tamasha lake la Pasaka lililozuiliwa kufanyika mjini Kampala, Arua and Lira kwa sababu za kiusalama.

Akizungumza na waandishi wa habari, msanii Nubian Li aliyekuwa  na Bobi wakati wa tukio hilo, amesema polisi walizuia msafara wa msanii huyo na kuwatawanya wafuasi wake ambapo walivunja dirisha la gari na kumtoa nje kisha kutokomea naye kusikojulikana.

Polisi wamelazimika kutumia mabomu ya machozi ili kuwatanya wafuasi wa Bobi waliokuwa wamefurika katika eneo hilo.

Agosti 27, mwaka jana, Wine na wanasiasa wengine 32 wa upinzani waliachiliwa huru kwa dhamana na Mahakama Kuu mjini Gulu, Kaskazini mwa nchi hiyo baada ya kushikiliwa kwa wiki kadhaa kufuatia mgogoro wa kisiasa nchini humo.

Watu wengine waliokamatwa ni waandaaji maarufu wa shoo za wasanii, nao ni promota Andrew Mukasa wa Bajjo na promota Abbey Musinguzi maarufu kama Abtex ambao walikuwa waandaaji wakubwa wa tamasha la Pasaka la Bobi lililokuwa lifanyike leo Jumatatu.

Msemaji wa Jeshi la Polisi nchini Uganda, Fred Enanga,  amekiri kukamatwa kwa Bobi na kumtoa katika maeneo ya Busabala lakini hakusema kama anashikiliwa na jeshi hilo ama la!

 

RC MWANRI Katangaza Vita na Madada Poa “Nitashuka nao jumla jumla”

Comments are closed.