The House of Favourite Newspapers

Bocco aleta balaa jipya Simba

JOHN Bocco nahodha wa Simba tayari ameanza matizi mepesi ndani ya siku saba atarejea uwanjani jambo ambalo linaongeza tabasamu la Kocha Mkuu, Patrick Aussems huku akiacha balaa kwa wachezaji
wenzake ambao watakuwa na vita ya kutafuta namba upya.

 

Bocco ni kipenzi cha Aussems kutokana na kuwa kwenye mfumo wake tangu msimu uliopita na aliwahi kuanza kwenye kikosi cha kwanza akiwa anaumwa katika mechi dhidi ya Coastal Union. Msimu huu hajacheza mchezo hata mmoja kutokana na kusumbuliwa na majeruhi.

SIMBA

Kwa namna mfumo wa Ausems ulivyo hali itakuwa ngumu kwa viungo ambao watakuwa wakigombania namba kwa kuwa walikuwa wakimshikia Bocco kwa muda. Mfumo wa 4-33 Aussems msimu huu mbele alikuwa anampanga Hassan Dilunga, Deo Kanda pamoja na Meddie Kagere ambaye yeye yupo kwenye mfumo huku wakati mwingine alimtumia Ajibu kwenye mchezo dhidi ya Biashara United.

 

Akiamua kutumia 4-4-2 mbele alikuwa anampa nafasi Sharaf Shiboub kwenye mchezo dhidi ya Kagera Sugar na alimtumia Clatous Chama kwenye mchezo dhidi ya Mtibwa Sugar hivyo kurejea kwa Bocco hapo kuna mchezaji lazima aanzie benchi kumpisha Bocco.

 

Aussems alisema kuwa wachezaji wote wa Simba ni sawa na wana kazi kubwa ya kufanya kwa ajili ya kutetea ubingwa na kwenye kila mechi anahitaji kuona timu ikishinda bila kujali nani anaanza. “Kila mchezaji kwangu ana umuhimu, hata Bocco pia ni mchezaji muhimu nina amini kurejea kwake kutaongeza ushindani na morali kwa wachezaji,” alisema Aussems

Comments are closed.