The House of Favourite Newspapers

Bocco: Lazima Tuwafunge Nkana

NAHODHA wa Simba, John Bocco amesema kuwa, wana kazi kubwa ya kufanya ili kuibuka na ushindi katika mchezo wa kesho Jumamosi dhidi ya Nkana FC kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika lakini lazima washinde.

 

Kesho Jumamosi, Simba itacheza na Nkana ukiwa ni mchezo wa kwanza utakaochezwa nchini Zambia wa Hatua ya Kwanza ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

 

Simba ambayo iliondoka juzi Juma­tano kwenda kucheza mchezo huo, inaisaka nafasi ya kutinga makundi ya michuano hiyo mikubwa Afrika kwa ngazi ya klabu.

 

“Tuna kazi kubwa ya kufanya mbele ya Nkana ili tuweze kuvuka hatua hii ambayo kila mmoja wetu hapa anata­mani kuona tunatinga makundi.

 

“Suala la kwanza hapa ni kushinda na si kitu kingine, hatufikirii matokeo men­gine tofauti, tunataka kufikia malengo yetu na ndiyo maana tunahitaji kushin­da,” alisema Bocco.

 

Ikumbukwe kuwa, baada ya mchezo huo wa kesho, timu hizo zinatarajiwa kurudiana Desemba 23, mwaka huu jijini Dar ambapo mshindi wa jumla atacheza Hatua ya Makundi. Atakaye­fungwa, ataenda kucheza mechi za mtoano kuwania kucheza Hatua ya Makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika

Comments are closed.