The House of Favourite Newspapers

Bodi ya Filamu Yaipa Ulaji Mwingine Bongo Muvi

0
Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu nchini, Dkt. Kiagho Kilonzo (katikati) akizungumza kwenye mkutano huo, kulia ni Mkurugenzi wa Vido App Justin Kisa na kushoto ni Mkurugenzi wa Maendeleo ya Filamu nchini, Emmanuel Ndumukwa.

 

 

UNACHOWEZA kusema ni kwamba tasnia ya filamu nchini imezidi kuupiga mwingi, hiyo ni baada ya jana, Bodi ya Filamu nchini kuingia makubaliano na kampuni ya Vido App Media ambayo itatumika kununua na kuuza kazi za filamu za kitanzania.

Akizungumza kwenye uzinduzi huo Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu nchini, Dkt. Kiagho Kilonzo amesema ujio wa Vido App ambayo ni soko la filamu za hapa nchini utaongeza thamani na kuboresha maisha ya watayarisha wa filamu hapa nchini.

Wasanii wa Bongo Muvi, Coletha Raymond na Frollah Mvungi wakifurahia jambo wakati mkutano huo ukiendelea.

 

 

“Hii ni Tv ya mtandaoni ambapo sasa watanzania wataweza kuangalia filamu za hapa nchini kupitia App hayo jambo linalotafsiri kuzidi kukua kwa soko la filamu za hapa nchini na hivyo tunaweza kusema sasa tunaupiga mwingi.

Msanii Madebe Lidai na Gabo Zigamba wakifurahi jambo kwenye uzinduzi huo.

 

 

Baada ya kuzungumza hayo naye Mkurugenzi Mtendaji wa Vido App, Justin Kisai alisema:

“Mimi ndiye mwanzilishi wa Vido App ambapo niliianzisha App hii baada ya kuona changamoto nyingi zilizokuwa zikitokea kwenye soko la filamu hapa nchini.

“Kama mnakumbuka awali kazi za filamu zilikuwa zikiuzwa kwenye VHS na baadae Dvd lakini kote huko kulitawaliwa na malalamiko ya wizi wa kazi hizo kwa namna mbalimbali ikiwemo (piracy) kunakili kopi kienyeji bila kuwahusisha wenye filamu zao  jambo lililowadidimiza sana na kuwakatisha tamaa watayarishaji wengi hapa nchini.

Mapaparazi wakiwajibika kazini katika tukio hilo.

 

 

“Sasa nimeanzisha App hii ambayo ni sawa na Inflix, Kipaji App, Sineza Zetu na nyinginezo ambazo lengo lake kuu ni kuboresha soko la filamu hapa nchini.

“Tutakuwa tukinunua kazi za wasanii na kuzionesha kwenye App yetu na mtazamaji itamgharimu shilingi 500 kwa kila filamu atakayoingalia”.

“Kwa upande wa mtayarishaji wa filamu hiyo yeye tutajadiliana naye bei na tukikubaliana ndipo tutaanza kuiweka hewani” alisema Mkurugenzi Justin.

Kwa upande wake msanii mkongwe wa Bongo Muvi, Coletha Raymond amesema anaishukuru sana bodi ya filamu kwa kuzidi kuwatafutia wadau wa ndani na nje kwa ajili ya kuiboresha tasnia yao ambayo kuna kipindi iliwakatisha tamaa kufikia watayarishaji wengine kuamua kujikita kwenye mambo mengine.

“Mimi nisema ukweli naishukuru sana Bodi ya Filamu kupitia Mkurugenzi wake Mtendaji Dkt Kilonzo kwa kuzidi kututafutia masoko ya kazi zetu jambo ambalo sasa linarudisha uhai wa kazi yetu na nawaomba wazidi kututafutia wadau zaidi ili kila mmoja achague mdau wa kufanya nae kazi kwa kuangalia wapi kuna maslahi” alisema Coletha.

Kauli ya Coletha iliungwa na wasanii wenzake Madebe Lidai, Gambo, Dude, Kupa na wengineo waliokuwa kwenye uzinduzi huo.

Leave A Reply