The House of Favourite Newspapers

Bodi ya Ligi iwe makini na Simba vs Yanga

WIKIENDI ijayo kutakuwa na mechi kali ya Simba na Yanga kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Huu ni mchezo ambao umekuwa ukizoa hisia za mashabiki wengi sana.

 

Lakini pia umekuwa ukitoa picha ya ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara kwa kuwa mara nyingi timu hizo ndiyo zimekuwa zikiwania ubingwa huo kwa miaka mingi. Ni vizuri Shrikisho la Soka

 

soka hapa nchini na hata nje ya nchi. Mara nyingi ni mchezo ambao umekuwa na hisia kali sana kutoka kwa mashabiki wa soka hapa nchini.

Tanzania (TFF), pamoja na Bodi ya Ligi wakahakikisha kuwa mchezo huu ambao utatazamwa na mashabiki wengi unakuwa wa kiwango cha hali ya juu. Bodi ya Ligi wanatakiwa kuhakikisha kuwa mwamuzi anayepewa mechi hii anaimudu kwa asilimia 100, lakini pia ni vyema tiketi zikiwa zinapatikana kwa urahisi ili kuwapa nafasi mashabiki wengi nafasi ya kuuona mchezo huu.

 

 

Comments are closed.