The House of Favourite Newspapers

Zahera Ataja Jinsi Yanga Wanavyohujumiwa

Kocha Mkuu wa Yanga, Mkongomani Mwinyi Zahera.

KOCHA Mkuu wa Yanga, Mkongomani Mwinyi Zahera amefunguka kuwa kwenye mechi zao za mzunguko huu wa pili wanakabiliana na ugumu wa hali ya juu kutokana na kupambana na zaidi ya timu moja wakiwa uwanjani.
Kocha huyo hadi sasa ameiongoza Yanga kukaa kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu Bara ikiwa na pointi 58 baada ya kucheza michezo 23.

Kocha huyo Jumamosi hii ataiongoza Yanga kwenye ‘Kariakoo Derby’ kupambana na wapinzani wao wa jadi, Simba kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar.


Kocha huyo amefunguka kwamba mechi zao za awamu hii zinakuwa ngumu kutokana na wapinzani wao wengine kuzicheza kwa kutumia timu ambazo wanapambana nazo.

Pamoja na kwamba Zahera hakutaja moja kwa moja lakini hapa anaaminisha kuwa Simba na timu zingine za nafasi za juu zimekuwa zikihujumu mechi zao kwa kuwa ndiyo wapinzani wao wakubwa kwenye ligi.


“Mechi zetu za awamu hii zinakuwa ngumu sana kwa sababu tunapambana na zaidi ya timu moja uwanjani. Timu yangu inafanya kazi kubwa kupambana na timu za wapinzani wetu kutokana na wao kucheza mechi za wapinzani tunaokutana nao uwanjani.

“Unajua hawa wachezaji wangu wana urafiki na wachezaji wa timu pinzani sasa wanaambiwa kwamba nyuma yao kuna timu ambazo zinacheza mechi zao kwa ajili ya kutufunga sisi, jambo ambalo linafanya iwe ngumu sana kupata ushindi katika mechi zetu,” alisema Zahera.

Kwenye mechi zake nne zilizopita za Yanga wameambulia pointi tano baada ya kufungwa 1-0 na Stand United, kisha sare ya 1-1 na Singida United, wakatoka suluhu na Singida United kabla ya kushinda mbele ya JKT Tanzania.

Said Ally, Dar es Salaam

Comments are closed.