The House of Favourite Newspapers

Bombardier Iliyozuiliwa Canada Yaachiwa, Ipo Njiani Kutua Tanzania

SERIKALI ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imewathibitishia wananchi kuwa ndege yake aina Bombardier Q400 iliyokuwa imezuiliwa nchini Canada imeruhusiwa kuondoka nchini humo na muda wowote kutoka sasa itawasili hapa  nchini.

 

Taarifa hiyo imetolewa na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu, Gerson Msigwa, leo Machi 30, 2018 kupitia ukurasa wake wa Twitter huku akiweka picha zilizokuwa zikionesha ndege hiyo wakati wa matengenezo ya mwisho kabla ya kuruhusiwa kuondoka.

 

 

“Ndege yetu aina ya Bombardier Q400, iliyokuwa imezuiliwa nchini Canada ilikwishaondoka Canada kuja Tanzania. Pia ndege kubwa nyingine tatu ( Bombardier CS300 mbili kutoka Canada na   Boeing 787-8 Dreamliner moja kutoka Marekani), zitawasili baadaye mwaka huu. Nawatakia Ijumaa Kuu njema”, amesema Msigwa.

 

Comments are closed.