The House of Favourite Newspapers

Bombeso Dance Group: Iyobo ametokea kwetu

0

1.Wakifanya yao ndani ya ukumbi huo.Wakifanya yao ndani ya ukumbi wa Vijana Kinondoni Dar.

2.Burudani kwa kwenda mbele.Burudani kwa kwenda mbele.

3.Wasanii wa kudansi wakiwa katika pozi baada ya mazoezi.Kundi hilo likiwa katika pozi.

4

5Pozi kwa kwenda mbele.

   KUNDI la kudansi lijulikanalo kama Bombeso Dance Group, linalofanya maonyesho yake kwa mialiko ya shughuli mbalimbali za kijamii, limesema kuwa dansa Moze Iyobo, anayefanya kazi kwa msanii nyota Nasibu Abdul  ‘Diamond Platnumz’ alitokea kwao.

Akichonga na mwandishi wetu, Meneja wa kundi hilo, Abubakar Ramadhani alisema lengo lao ni kukuza vipaji vya vijana na kuwatia moyo katika kujikwamua kimaisha ambapo ili kuwa mwanachama, ni lazima mtu ajiandikishe kwa kujaza fomu maalum.

“Tunapata mialiko katika sherehe mbalimbali kama harusi, semina na makongamano ambako kazi yetu kubwa huwa ni kutoa burudani kwa waalikwa, kutokana na kufanya kwetu vizuri, tumekuwa tukipendwa sana na wadau,” alisema Ramadhani.
Alisema kundi lao lipo muda wowote katika ukumbi wa vijana likifanya mazoezi ili kujiimarisha kukabiliana na burudani zinazojitokeza huku akitaja mawasiliano yake kwa wanaolihitaji kundi hilo kwa ajili ya kutoa burudani, 0713870209

Na Denis Mtima/Gpl

Leave A Reply