The House of Favourite Newspapers

Bomoabomoa Yapitia Kanisa la Nabii Bilionea Sinza -(VIDEO)

0
Nabii John Billionaire.

NABII John Billionaire wa Kanisa la Shalom Tebanacle la Sinza Legho lililobomewa asubuhi ya leo, ameeleza hasara aliyoipata kutokana na kanisa lake hilo kubomolewa.

Akizungumza na Global TV Online, mchungaji huyo amesema kanisa lake lilikuwa hapo kwa miaka minne ambapo bomoabomoa imekuja pasipo na taarifa yoyote kuhusu ubomoaji huo.

Nabii huyo ameongeza kwa kusema kuwa hakuwahi kujua kama eneo hilo lilikuwa na mgogoro huku akielezeza kuwa hata mwenye nyumba hakuna na taarifa na kama angekuwa nayo angewapa notsi.

Amekwenda mbele kwa kueleza kuwa, suala hilo atalifuatilia kisheria zaidi kwa sababu suala la kiroho huwa haliji kwa ‘surprise’ akimaanisha kushtukiza!

VIDEO: Kanisa la Mchungaji Bilionea Labomolewa Sinza

Leave A Reply