The House of Favourite Newspapers

Bondia Mfaume Mfaume Bingwa Mpya wa WBF Afrika, Amtwanga Mmisri TKO

0
Bondia Mfaume Mfaume akiwa na mataji yake

 

Bondia wa ngumi za kulipwa nchini, Mfaume Mfaume amefanikiwa kushinda mkanda wa WBF Afrika kwa TKO ya raundi ya pili dhidi ya Abdumonem Said kutoka nchini Misri katika pambano la ubingwa la raundi kumi.

Mfaume ameshinda mkanda huo wa ubingwa WBF kwa mara ya kwanza baada ya kupita siku 444 bila ya kupanda ulingonni tangu alipopigwa kwa TKO ya raundi ya pili nchini Urusi.

Mabondia wakipepetana katika mapambano ya utangulizi

Katika pambano hilo ambalo limepigwa juzi Usiku kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee uliopo Upanga, Dar ambapo bondia huyo aliweka rekodi ya kushinda kwa TKO ya raundi pili wakati Ibrahim Class yeye amemchapa kwa TKO, Peter Pambani kutoka Zimbabwe kwenye raundi pili.

Juma Choki ameendeleza rekodi ya ubabe baada ya kumchakaza kwa pointi Issa Namepepe wakati Oscar Richard akimchapa kwa pointi Bongani Makovora huku Hamis Maya akishinda kwa tabu sana dhidi ya Mardochee Katembo kutoka DR Congo.

 

Mabondia wakipepetana katika mapambano ya utangulizi

Mwanadada, Stumai Muki amefanikiwa kushinda kwa pointi dhidi ta Nicholine Achieng lakini Pius Mpenda amefanikiwa kumtandika kwa KO George Dimoso huku Laurent Segu akimaliza shughuli kwa kumchapa kwa pointi Thomas Haule.

 

Leave A Reply