The House of Favourite Newspapers

Bora RX Medicina Yatumia Sh Milioni 46 Kukarabati na Vifaa vya Kituo cha Afya Gerezani

0
Margareth Maganga, Mkurugenzi Mtendaji wa Bora Rx Medicina akizungumza baada ya kutoa vifaa hivyo.

 

IJUMAA, Novemba 24, 2022 DAR ES SALAAM — Kampuni ya Bora Rx Medicina imetoa msaada wa vifaa vya kisasa vya matibabu na kufanya ukarabati katika Kituo cha Afya cha Gerezani kilichopo wilayani Ilala. Thamani ya msaada huu ni zaidi ya shilingi milioni 46.

 

“Kila mfanyakazi wa afya nchini Tanzania anahitaji vifaa vya kisasa na vya uhakika ili kutoa huduma bora za afya kwa wagonjwa,” alisema Morris Mwinuka, Mfamasia kutoka Bora Rx Medicina.

Mkurugenzi Mtendaji wa Bora Rx Medicina Margareth Maganga wa (pili kutoka kulia) akikabidhi moja ya vifaa hivyo kwa mgeni rasmi Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Ng’wilabuzu Ludigija (katikati mwenye suti) Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala (kulia) na viongozi wengine waliohudhuria tukio hilo.

 

Msaada huo toka kampuni inayomiliki maduka ya dawa utasaidia kuimarisha mfumo wa afya ya jamii katika wilaya ya Ilala. Bora Rx Medicina ilifanya ukarabati wa maabara, vyumba viwili vya uchunguzi, duka la dawa, ofisi ya muuguzi mkuu, vyoo na ofisi za wafanyikazi.

 

Katika hotuba yake Morris Mwinuka, mfamasia wa Bora Rx Medicina alisema vifaa vilivyotolewa ni pamoja na vitanda vitano vya kufanyia uchunguzi, kitanda kimoja cha wodini, samani, darubini, immunoassay analyser, centrifuge, semi-auto biochamp, coaqulation machine, urine analyser, electrolyte analyser, FBP analyser, water bath, and incubator.

Mkuu wa Wilaya ya Ilala Ng’wilabuzu Ludigija na Mkurugenzi Mtendaji wa Bora Rx Medicina wakiongoza tukio kukata utepe.

 

Msaada huu utasaidia zaidi ya wagonjwa 10,000 wa Zahanati ya Gerezani iliyopo katikati ya soko kubwa la Kariakoo.

 

Mwinuka alisema msaada huo unalenga maeneo muhimu katika sekta ya afya nchini Tanzania ambayo serikali imewekeza kwa kiasi kikubwa. “Tunatumai kuwa shughuli yetu hapa Gerezani itasaidia wanawake na watoto kupata huduma bora za matibabu.”

Sehemu ya vifaa hivyo.

 

Mnamo mwaka wa 2022, serikali ilitenga takriban shilingi trilioni 1.1 kwa ajili ya ununuzi wa dawa, vifaa tiba na usambazaji. Hivi karibuni, juhudi za serikali katika sekta ya afya zimejumuisha chanjo kwa watoto, kuongeza vitamini A, kuzuia maambukizi ya VVU kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto, na uboreshaji wa udhibiti wa magonjwa ya utotoni. Mipango hii imeokoa maisha ya maelfu ya wananchi wanaofaidika zaidi wakiwa ni wanawake na watoto.

 

“Bora Rx Medicina inajivunia sana kuweza kusaidia Wizara ya Afya katika kuboresha huduma za afya nchini Tanzania,” Mwinuka alisema. “Tutashirikiana na serikali katika nyakati hizi za wasiwasi mwingi wakati ulimwengu unakabiliwa na changamoto nyingi za kiafya.”

Baadhi ya vifaa vilivyotolewa na kampuni hiyo.

 

Katika hafla ya makabidhiano, Mhe. Ng’wilabuzu Ludigija, Mkuu wa Wilaya ya Ilala alisema: “Vitu hivi vimekuja kwa wakati mwafaka. Vitasaidia juhudi zetu za kuimarisha mfumo wetu wa afya. Lengo letu ni kuhakikisha kwamba kila mgonjwa anayetembelea vituo vyetu vya afya anapata huduma anayostahili.”

 

Ludigija alisema mchango huo ni mfano wa mzuri wa ubia kati ya serikali na sekta binafsi unaonufaisha watu. “Tunajivunia kushirikiana na Bora Rx Medicina na kuweza kuwategemea kama mshirika wetu wa kimkakati katika kufikia lengo la: kuokoa maisha.”

 

Akijibu maoni ya Ludigija, Margareth Maganga, Mkurugenzi Mtendaji wa Bora Rx Medicina alisema kampeni hiyo itaendelea kushiriki kikamilifu katika mipango yote ya afya ya serikali kwa kuwezesha upatikanaji wa dawa na vifaa vya afya nchini.

 

“Tutajitahidi kutimiza ahadi ya jina letu (Bora). Tutafanya kila kilicho ndani ya uwezo wetu kuisaidia serikali katika juhudi zake njema za kuleta huduma bora za afya kwa Watanzania”.  Alimaliza kusema Maganga.

Leave A Reply