The House of Favourite Newspapers

Bosi amfanyia umafia hausigeli wake!

0

house girl (2)

Mariamu akionesha jeraha lililopo mbavuni.

UMAFIA  wa kutisha!  Dada mmoja aliyefahamika kwa jina la Mariamu mkazi wa Mwananyamala jijini Dar, amefanyiwa umafia kama siyo unyama wa kutisha na bosi wake aliyekuwa akimfanyia kazi za ndani.

Mariam aliliambia gazeti hili juzi kuwa, tukio hilo lilitokea usiku wa Jumapili ya Septemba 13, mwaka huu nyumbani kwa bosi wake huyo aitwaye David maeneo ya Kinondoni jijini Dar.

house girl (1)Jeraha jingine karibu kwenye mkono.

Msikie Mariam

“Ilikuwa ni kawaida yangu kila Jumapili kwenda nyumbani kwake kumfanyia shughuli za usafi kwa malipo ya shilingi 10,000 mara nyingine 15, 000 sasa tofauti na siku zote, Jumapili hii nilipokwenda nilimkuta akiwa na mgeni aliyenitambulisha kuwa ni mdogo wake.

house girl (1)1“Nikafanya shughuli zangu za usafi kama kawaida, baada ya kumaliza nilimuaga na kuondoka maana mimi pia huwa ni mshereheshaji sasa kulikuwa na dili nilikuwa naenda kulifanya.

“Nikiwa kwenye sherehe, bosi wangu huyo alinipigia simu na kunitaka nirudi maana kulikuwa na upotevu wa simu. Nikamjibu kuwa sijaichukua mimi lakini hakunielewa, ndipo nikaamua kwenda nyumbani kwake.

Alipofika ikawaje?

“Nilipofika alinichukua yeye na mdogo wake na kuanza kunishambulia kwa kunipiga na mabapa ya panga huku akinitaka nioneshe mahali nilipoificha simu hiyo. Nilizidi kujitetea kuwa sikuchukua lakini hakunielewa, akazidi kunitesa.

“Akaniingiza kwenye chumba f’lani na kunivua nguo kisha akawa ananipiga kwa bapa la panga ambapo alinikata mgongoni. Wakachukua pasi yenye moto na kunichoma sehemu mbalimbali mwilini, walinitesa sana.”

Apata upenyo

“Kuna wakati waliniacha kwenye chumba hicho ndipo nilipowapigia simu ndugu zangu na kuwataka waje haraka ikiwezekana na polisi. Hata hivyo, walishindwa kuwapata polisi ila walikuja wenyewe na kunikuta nimeshatolewa nje na kuambiwa niondoke haraka.

Breki ya kwanza polisi

Mariamu alizidi kueleza kuwa, kutokana na hali aliyokuwa nayo ndugu zake walimshauri kwenda kutoa taarifa kwenye Kituo cha Polisi Oysterbay.

“Tulienda pale polisi Oysterbay, tukaandika maelezo kisha tukapewa fomu kwa ajili ya matibabu (PF3) na kufungua RB yenye namba: OB/RB/14593/2015, KUJERUHI kisha nikaenda hospitali ambako nilitibiwa ikiwa ni pamoja na kushonwa nyuzi 18 mgongoni na 16 mkononi,” alisema Mariam.

Jitihada za kumpata mtuhumiwa huyo hazikuzaa matunda ila taarifa za kipolisi zimethibitisha kukamatwa kwa bosi huyo.

JIUNGE NA GLOBAL BREAKING NEWSglobalbreakingnews.JPG

 

Leave A Reply