The House of Favourite Newspapers

Bosi: Kwa Simba Hii, Mtaachia Kila Kitu… Luis, Kramo, Onana, Ngoma na kipa kutoka Brazil

0
Wachezaji wa Simba wakiendelea na mazoezi.

UONGOZI wa Simba umeweka wazi kuwa usajili ambao wameufanya msimu huu unastahili kwao kufanya vyema msimu ujao haswa kuyarudisha mataji yote ambayo wameyapoteza kwa misimu kadhaa.

Simba mmpaka sasa wamefanya usajili wa wachezaji wa maana wa kimataifa kama Luis Miquissone, Aubin Kramo, Essomba Onana, Fabrice Ngoma na kipa kutoka Brazil, Jefferson Luis.

Luis Miquissone

Akizungumza na Championi Jumatano, Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Simba, Ahmedy Ally alisema kuwa kwa majembe ambayo wamayashusha yakiongozwa na Luis Miquissone ni wazi kuwa matarajio yao ni kuhakikisha kuwa wanabeba mataji yote msimu ujao ambayo waliyapoteza kwa kuwa watakuwa na kikosi bora.

“Huu usajili ambao tumeufanya ni balaa tupu kwani majembe ambayo tumeyashusha ni wazi kuwa msimu ujao kazi yetu itakuwa kuhakikisha kuwa tunayarudisha mataji yetu yote ya ndani ambayo tuliyapoteza misimu miwili iliyopita.

Kipa kutoka Brazil, Jefferson Luis.

“Wapinzani wetu wajiandae kwani safari hii tumeshusha vyuma ambavyo vinaakisi nini tunahitaji msimu ujao katika kila mashindano ambayo tutashiriki, kuanzia mashindano ya ndani mpaka yale ya nje,” alisema kiongozi huyo.

Stori Na Marco Mzumbe

ABBAS TARIMBA AFUNGUKA SAKATA la MAYELE KUUZWA – “NIMEFURAHI, FEI TOTO SIJAKUBALIANA NAYE”..

Leave A Reply