The House of Favourite Newspapers

Boxer Abadili Mfumo Yanga

Paul Godfrey ‘Boxer’

KUTOKANA na kuumia kwa beki Paul Godfrey ‘Boxer’ kumemlazimisha Kocha Mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera kubadili mfumo wa 4-4-2 na kwenda 3-5-2, huku kiungo mshambuliaji Balama Mapinduzi akipewa majukumu ya kucheza nafasi hiyo.

 

Kocha huyo amelazimika kutumia mfumo huo wakati wakijiandaa na mchezo wao wa kesho Jumamosi wa Ligi ya Mabingwa Afrika ambao watacheza na Zesco United kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar.

 

Kocha huyo mwenye uraia pacha wa DR Congo na Ufaransa ameliambia Championi Ijumaa, kuwa analazimika kumtumia Balama kwenye nafasi hiyo ya ulinzi kutokana na mabeki wake wanaocheza nafasi hiyo kutokuwa sawa.

 

“Hadi sasa kuna shida kwenye upande wa beki wa kulia kwani Boxer aliumia kwenye ile mechi na Ruvu Shooting wakati Juma Abdul hakuwa kwenye pre-season, hivyo anahitaji muda zaidi kujiandaa.

 

“Kwa hiyo unaona kabisa ndiyo maana kwa sasa ninamjaribu Mapinduzi kwenye nafasi hiyo na tayari nimeshamchezesha katika mechi zetu mbili zilizopita na amefanya vizuri.

 

“Kwa sababu tutatumia mfumo mwingine wa 3-5-2 kwa hiyo wale mawinga ndiyo wanakuwa mabeki na kutokana na pumzi ya Balama ndiyo maana ninamchezesha kama beki wa kulia, lakini majibu ya kwamba nitamtumia kwenye nafasi hiyo nitayapata kwenye mazoezi ya kesho (leo) Ijumaa kwani ndiyo yatakuwa ya mwisho,” alisema Zahera.

SPOTI HAUSI: NJIA Za YANGA Kutoa ZESCO UNITED Ni HIZI..!

Comments are closed.