The House of Favourite Newspapers

ESTER BULAYA Aibua Kashfa Ya Deni La Serikali Trilioni 8 – Video

Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimepinga sheria mpya ya mafao ya hifadhi ya jamii kikidai sheria hiyo inamuumiza mtumishi Mwenye kipato cha chini katika mafao yake pindi anapostaafu.

 

Akizungumza na waandishi wa habari kwenye ofisi za Makao makuu ya Chama hicho, Waziri kivuli Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Esther Amos Bulaya amesema sheria hiyo inampa mtumishi 25% ya mafao Yake pindi akistaafu huku 75% akilipwa ndani ya mshahara wake akiwa Kazini.

 

Bulaya amesema Serikali imekuwa ikikopa na kuchelewesha mafao ya wastaafu ambapo mpaka sasa serikali inadaiwa takriban trillion 8 na mifuko hiyo na kusisitiza ni Wajibu wa serikali kulipa Pesa hizo kwa maslahi ya wastaafu.

 

Hata hivyo amegusia suala la Ajira na kupanda kwa madaraja na mishahara kwa watumishi ambapo amesema kwa kipindi cha miaka 3 serikali imeshindwa kuajiri na kupandisha mishahara kwa watumishi hali inayopelekea ongezeko la vijana wasio na Ajira mtaani.

 

Bulaya ameishauri Serikali kama Waziri kivuli Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu na kuwataka wafuate ushauri huo kwa maslahi mapana ya Taifa.

 

MSIKIE HAPA AKIFUNGUKA

Comments are closed.