The House of Favourite Newspapers
gunners X

Breaking: CCM Yampitisha Mwinyi Kugombea Urais Zanzibar

0

 

MKUTANO wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi  (CCM) Taifa umemteua Dkt. Hussein Mwinyi kuwa mgombea urais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

 

1. Dkt Hussein Ali Hassan Mwinyi  alipata kura 129 (78.65%)

2. Dkt Khalid Salim Mohamed -kura 19 (11.58%)

3. Shamsi Vuai Nahodha -kura 16 (9.75%).

 

Akizungumza jijini Dodoma mara baada ya kutangazwa mshindi na kupewa ridhaa ya kugombea urais wa Zanzibar,  Mwinyi amesisitiza ushirikiano na mshikamano ndani ya chama hicho wakati huu wa kuelekea uchaguzi mkuu mwezi Oktoba mwaka huu.
Amesema ushirikiano na mshikamano ndiyo utakaokiwezesha chama hicho kupata ushindi wa kishindo katika uchaguzi mkuu ujao kwa pande zote mbili za muungano.

Leave A Reply