The House of Favourite Newspapers

BREAKING: NYALANDU, WENZAKE WAACHIWA KWA DHAMANA

 

ALIYEKUWA Mbunge wa Singida Kaskazini na kada wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Lazaro Nyalandu na wenzake wawili wameachiwa kwa dhamana ya polisi kwa masharti kwamba  hao wawili wadhaminiwe na wadhamini wawili, na Lazaro Nyalandu awe na  wadhamini watatu kwa Sh. milioni tano kila mmoja na wanatakiwa kuripoti polisi Singida mjini kesho asubuhi saa 3.

 

Mkuu wa taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) mkoani Singida, Joshua Msuya,  alisema walipata taarifa za uwepo wa viashiria vya rushwa kwenye mikutano ya moja ya vyama vya siasa mkoani humo baada ya kufuatilia ndipo walimkuta Lazaro Nyalandu akiwa katika nyumba moja ambayo si ofisi ya Chadema akiendesha kikao.

Comments are closed.