The House of Favourite Newspapers

BREAKING: Lipumba Anga’ka! Wanachama Wake Kukamatwa Kibiti! – VIDEO

Mwenyekiti wa Chama Cha Wananchi (CUF), Prof. Ibrahim Lipumba amelaani vikali tukio la viongozi wake wa Wilaya ya Kibiti na Mkuranga waliodaiwa kukamatwa na jeshi la polisi wakati wakirudisha fomu za chaguzi za udiwani kwenye kata mbalimbali kwa madai ya kuwa fomu walizokuwa wakizirudisha niza kugushi.

 

Hayo ameyaeleza leo jijini Dar es Salaam wakati wa kufungua Kikao cha Baraza la Viongozi wa CUF ambapo katika matukio hayo amelaani kitendo hicho kilichofanywa na jeshi hilo na akaeleza kuwa ushahidi matukio hayo anao kwani baadhi ya viongozi walioachiwa wapo na ataelekea nao katika ofisi za tume ya Taifa ya uchaguzi kuieleza kilichotendeka huko Kibiti.

 

Mbali na hayo pia amedai kuwa wananchama wanaohamia Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa madai ya kwamba wamefuata sehemu ilipo demokrasia ya kweli na kuunga juhudi zinazofanywa na chama tawala si za kweli kwani hali ya maisha ya watanzania si nzuri hususani ya ki biashara na upatikanaji wa pesa umekuwa mgumu.

 

Video: Lipumba Akifunguka

Comments are closed.