The House of Favourite Newspapers

BREAKING: Makonda Atangaza Msako Wacheza Filamu za Ngono Dar – Video

Mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaam, Paul Makonda ameunda Kamati ya watu 17 ya kuchunguza masuala mbalimbali yanayofanywa na baadhi ya vijana wa Mkoa huo kinyume na sheria na desturi za nchi ikiwemo wanaocheza filamu za ngono, ushoga, utapeli wa mapenzi, makundi ya ngono kwenye WhatsApp na nyumba zinazotumika kurekodia video za ngono.

 

Makonda ameyasema hayo leo wakati akizungumza na wanahabari Ofisini kwake jijini Dar es Salaam ikiwa ni siku tangu alipowataka wakazi wa Dar kumtumia majina ya watu wanaojihusisha na vitendo hivyo baada ya video ya msanii Amber Rutty kusambaa mitandaoni akifanya mapenzi kinyume cha maumbile.

 

“Kwa kujua yatakuwa Makao Makuu ya nchi, kuna machangudoa tayari wametoka Dar es Salaam na kwenda Dodoma ili kuona kama soko lao litapatikana kule, wengine wameanzisha madanguro yao Bagamoyo, Mpanda, Arusha na sehemu nyingine hili jambo hata Mungu hawezi kukubali. 

 

Tumeamua kuunda kamati itakayokuwa na majukumu manne, moja itakayo-deal na kundi lote la mashoga, wanaojitangaza na wale wasiojitangaza lakini wanajulikana ni mashoga.  Tutashughulika na watu wote wanaocheza picha za ngono, hapa Dar kuna nyumba 24 zinazotumika tumeshazifahamu, wanachukua madada wanawaleswesha madawa kisha wanawafanyisha, wengine wanaingia makubaliano, wanawalipa kisha kuwarekodi na kuziuza. 

 

“Tutashughulika na watu wote wanaojitangaza kujiuza kupitia mitandao ya kijamii. Kuna kundi la la linafanya biashara ya ngono, matukio yote ya ngono unayapata huko, nimeshapata namba za huyo dada ambaye ni admin wa hilo kundi. 

 

“Pia Tutashughulika na watu wanaotumia mitandao kutapeli, wanatumia majina ya viongozi wakuu wanchi wakiwemo majina ya Rais, Makamu wa Rais, Waziri Mkuu kutapeli. Wengine wanasema wametumwa na Makonda, wapo ambao tayari tumeshawakamata” alisema RC Makonda.

 

MSIKIE MAKONDA AKIFUNGUKA HAPA

Comments are closed.