The House of Favourite Newspapers

BREAKING: MCHUNGAJI MASHIMO AWADHAMINI AMBER RUTTY, MPENZI’YE – VIDEO

HATIMAYE nyota wa video (video vien) za  Bongo, Nascat Abubakary ‘Amber Rutty’ na ‘bwana’ke’, Said Mtopari, wameachiwa kwa dhamana katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam leo, Novemba 27, 2018 mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Augustine Rwizire.

Wawili hao wameachiwa huru mapema leo baada ya kutimiza masharti ya dhamana ambapo Amber Rutty amedhaminiwa na ndugu yake aitwaye Salma Omary Bungo (46), na Asha Mohammed (46) huku anayedaiwa mpenzi wake, Mtopari akidhaminiwa na  Mchungaji Daud Mashimo wa Kanisa la Emmaus Bible Church la Mbezi Luis Dar es Salaam na Francis Chacha.

Masharti ya mahamama yaliwataka kila mmoja kuwa na wadhamini wawili ambapo kila mmoja amesaini bondi ya Sh. milioni 15, pia wametakiwa kuwa na vitambulisho vya taifa pamoja na kuwasilisha hati zao za kusafiria.

Aidha mahakama imewaamuru watuhumiwa hao wasitoke nje ya Dar es Salaam bila kibali cha mahakama.

Amber Rutty na Said Bakary walifikishwa mahakamani hapo Novemba 2, mwaka huu wakikabiliwa na mashtaka matatu yakiwemo ya kufanya mapenzi kinyume na maumbile na kusambaza picha za ngono kupitia mitandao ya kijamii ambapo kesi yao iliahirishwa jana Desemba 10, mwaka huu.

Mbali na Amber Rutty na Said Bakary ambao walishindwa kudhaminiwa kwa mara tatu mfululizo,  mshtakiwa mwingine katika kesi hiyo ni James Charles maarufu kama ‘James Delicious’ ambaye  alishadhaminiwa.

Comments are closed.