The House of Favourite Newspapers

DC Mwanziva Abeba Agenda ya Kumtua Mama Ndoo Lidewa, Aweso Apiga Simu Kutoa Kauli ya Wizara ya Maji

0

Mkuu wa wilaya ya Ludewa Victoria Mwanziva amewataka watendaji kata pamoja na madiwani kuungana na ajenda ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan iliyolenga kumtua mama ndoo kichwani kwa kufuatilia utekelezaji wa miradi ya maji inayoletwa katika maeneo yao na kuhakikisha inakamilika na kotoa maji yaliyo safi na salama.

Mkuu huyo wa wilaya ameyasema hayo katika jukwaa la wadau wa maji wilayani humo lililofanyika 05/05/2024 na kuhusisha Kamati ya Usalama, kamati ya siasa ya chama cha mapinduzi,madiwani, maafisa Tarafa, watendaji kata pamoja na timu ya wataalamu (CMT) Wilayani humo.

“Mheshimiwa Rais amefanya kazi kubwa sana wilayani kwetu kwani kwa sasa tuna miradi Saba ya maji yenye thamani ya zaidi ya Bilioni 13.8 ambayo inaendelea kutekelezwa hivyo viongozi wa ngazi zote tunapaswa kusimamia fedha hizi ili zitumike ipasavyo na kuhakikisha miradi inatoa huduma stahiki”. Amesema Mwanziva.

Ameongeza kuwa jukwaa hilo limeandaliwa madhubuti ili kujadili na kuhoji changamoto zilizopo katika miradi mbalimbali na kuweza kuzitatua ili kuwaondolea wananchi changamoto zinazowapelekea kutembea umbali mrefu kufuata maji kwakuwa maji ni muhimu na hayana mbadala.

Aidha Waziri wa Maji Mhe Jumaa Aweso amezungumza na viongozi wa Wilaya ya Ludewa kwa njia ya simu kuwasalimu wadau wa sekta ya Maji Ludewa na kuwahakikishia kuwa wilaya hii itapewa kupaumbele katika kumaliza changamoto ya Maji na kutoa kauli juu ya wizara ya Maji kukamilisha Miradi inayoendelea.

Pia ametoa wito na ukaribisho kwa Mkuu wa Mhe Wilaya ya Pangani na Mhe Mbunge wa Jimbo la Ludewa sambamba na mkandarasi anaetekeleza mradi mkubwa mji wa Ludewa wa Bilion 7.4 unaohusisha ujenzi, upanuzi na ukarabati kufika wizarani Dodoma na kuweka mpango madhubutu wa kuukamilisha haraka kwani mradi huo ukikamilika utapelekea eneo hilo la mji kupata maji kwa asilimia 95%.

Katika hatua nyingine akizungumza na Wana Ludewa Waziri Aweso Amesema RUWASA Wilayani humo imepokea kiasi cha Sh. Bilioni 1.30 ambapo kiasi cha Sh. Milioni 300 zitatumika katika uchimbaji wa visima na millioni 700 zitatumika kukamilisha baadhi ya miradi ambayo inatarajiwa kukamilika kabla ya Juni 30 mwaka huu.

Leave A Reply