The House of Favourite Newspapers

BREAKING: Ndugu Wasusa Kuzika Mwili wa Ndugu Yao, Polisi Wafunguka

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kipolisi wa Temeke, Emmanuel Mkula, amezungumza na waandishi leo na kutolea ufafanuzi kuhusu na sakata la ndugu kugoma kumzika ndugu yao ambaye mwili wake kwa sasa upo katika Hospitali ya Taifa, Muhimbili kwa kile wanachodai kutaka maelezo kutoka polisi juu ya kilichosababisha kifo cha ndugu yao huyo.

 

RPC Mkula amesema kwa mara kadhaa kumekuwa na matukio ya ujambazi na uporaji wa kutumia silaha ambapo baada kukithiri kwa vitendo hivyo, Kamanda wa Kanda Maalum ya DSM, Lazaro Mambosasa akatoa maagizo kwa Makamanda wa polisi wa mikoa ya kipolisi mitatu, Ilala, Kinondoni kuandaa kikosi kazi cha kupambana na majambazi.

 

RPC Mkula amesema siku ya Agosti 11, Mkuu wa Upelelezi wa wilaya ya Chang’ombe alipokea taarifa kwamba eneo la Claudia Motel Kiwalani, kuna watu wanne wamefika wakiwa na mfuko mwekundu mkubwa unaodaiwa kuwa na silaha aina ya Bastola.

 

Polisi walipopata taarifa walifika haraka eneo hilo kwa lengo la kutaka kuwabaini watu hao, na walipofika waliwakuta watu hao wakiwa katika mgahawa huo ambapo walijitambulisha na wakiwa katika harakati za kuwakamata ili wakafanye nao mahojiano zaidi ndipo mmoja kati ya watuhumiwa hao, Salum Kindamba, alikurupuka na kukimbia akiwa na mfuko huo.

 

Askari walimtaka asimame na kufanya juhudi zote na taratibu za kisheria ikiwemo kufyatua risasi hewani na kupiga filimbi ili asimame ambapo juhudi hizo zote ziligonga mwamba kwani mtuhumiwa huyo aliendelea kukimbilia vichochoroni ambapo polii ikawabidi kumfyatulia risasi iliyomlenga maeneo ya Kiunoni na kumuangusha chini ambapo alikimbizwa hospitali ya Mkoa wa Temeke na baadaye akapoteza maisha.

MSIKIE RPC AKIFUNGUKA

Ndugu Wa Marehemu Wakataa Kuchukua Maiti, Wadai Polisi Wamemuua

Comments are closed.