The House of Favourite Newspapers

Breaking News: Askofu Gwajima Atembelea Clouds Kuwapa Pole Baada ya Kuvamiwa na Makonda (VIDEO)

Askofu wa Kanisa la Ufufuno na Uzima, la Jijini Dar es Salaam, Mch. Josephat Gwajima amewatembelea na kuwapa pole wafanyakazi wa Kituo cha televisheni cha Clouds TV baada ya kituo hicho kuvamiwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam mwishoni mwa wiki iliyopita akiwa ameandamana na askari wenye bunduki.

 

Katika tukio inadaiwa kuwa Makonda alifika Clouds na kuwashinikiza watangazajia wa kipindi cha Da Weekend Chat Show (Shilawadu) warushe hewani kipindi ambacho kilikuwa kimerekodiwa kikimuonesha mama aliyedaiwa kuwa amezaa na Gwajima kisha kumtelekezwa mama huyo pamoja na mtoto wake.

Gwajima amewapa pole Clouds Media na kuwataka wawe wavumilivu huku akiwasihi kuwa yote yaliyotokea ni mipango ya Mungu.

Baadhi ya maneno aliyozungumza Gwajima

“Sina ugomvi binafsi na RC Makonda lakini nilichokifanya nikuwa nafafanua ukweli ili Rais Magufuli achukue hatua zinazostahili dhidi yake. Mimi sio mwanasiasa, sina nia na Jimbo la Misungwi, kama yeye anataka Ubunge aendelee.”

“Binti aliyelishwa maneno aseme nimezaa nae, yupo Ustawi wa Jamii akiandika maelezo kuwa maneno aliyoyatoa ni ya uongo. “Nina watoto watatu wa ndani ya ndoa… Sina mtoto mwengine.” 

“Mh.Paul Makonda atatoa vyeti vyake kwa wakati wake mwenyewe. Sijaja hapa kuwagombanisha Clouds na Serikali, nimekuja kuwapa pole hayo mengine tuyaacha kama yalivyo. Nipo hapa leo kwa ajili ya kuwapa pole Clouds.” Alisema Gwajima.

TAZAMA VIDEO ALICHOKIZUNGUMZA GWAJIMA

Comments are closed.