The House of Favourite Newspapers

BREAKING NEWS: Magari 10 Yateketea Kwa Moto Rusumo, Kagera -Video

 

MAGARI kadhaa yameteketea kwa moto leo baada ya lori la mafuta la kampuni ya Ratco kufeli breki na kugonga magari mengine kumi yaliyokuwa yanapakia pumba katika eneo la Rusumo mkoani Kagera.

 

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kagera, Augustino Olomi, amethibitisha tukio hilo na amesema  wanaendelea na jitihada za kuuzima moto huo uliokuwa unaendelea hadi mchana ambao ulioanza saa tatu asubuhi baada ya magari mawili kugongana eneo hilo wilayani Ngara.

 

Alisema uchunguzi wa chanzo halisi cha tukio hilo utafanyika baada ya kukabiliana na moto huo.

 

“Tutatoa taarifa rasmi ya chanzo cha moto huo, kwa sasa tunaendelea kuuzima. Ni tukio la kushangaza maana eneo hilo magari kila siku yapo na yanapita, hivyo lazima tufanya uchunguzi kubaini ukweli wa chanzo cha moto, huo, ” alisema.

 

Awali Michuzi Blog ilitoa taarifa za awali kuhusu kuungua moto kwa magari katika eneo la Rusumo jirani na Ofisi za Idara ya Uhamiaji ambazo zipo mpakani kwa Tanzania na Rwanda.

Comments are closed.