The House of Favourite Newspapers

Breaking News: Muuza Genge Ajinyakulia Pikipiki, Zawadi Kibao Zatolewa

Droo ya kwanza ya shindano la Tusua Maisha na Global, imefanyika na kurushwa live na kituo cha runinga cha Global TV Online ambapo Richard Tanganyika, mfanyabiashara ndogondogo anayemiliki genge katika eneo la Mdaula, Chalinze mkoani Pwani ameibuka mshindi.

 

Akizungumza na Gazeti hili, Richard amefunguka kwamba awali alikuwa haamini kama anaweza kuibuka mshindi na kuishukuru sana kampuni ya Global Publishers kwa kuyabadili maisha yake.

“Naishukuru sana kampuni ya Global Publishers na nawaomba watu wengine wasome magazeti kwani ni kweli unaweza kushinda. Mimi hakuna mtu yeyote tunayefahamiana naye Global au ndugu yangu lakini nimeshinda, ni jambo la kumshukuru sana Mungu,” alisema Richard ambaye atakabidhiwa zawadi yake siku chache zijazo.

 

Alipoulizwa ataitumia vipi pikipiki hiyo, Richard amesema anatarajia kuitumia kuendeshea biashara zake, ikiwa ni pamoja na kufuata bidhaa za genge lake. Washindi wengine waliopatikana katika droo ya kwanza, wamejishindia jezi, dinner set pamoja na headphones za kisasa za Beats by Dre.

“Kila mmoja anaweza kuwa mshindi, namna ya kushiriki kwenye Shindano la Tusua Maisha na Global, ni rahisi, nunua gazeti lolote linalochapishwa na Global Publishers, kati ya Uwazi, Risasi, Amani, Ijumaa, Ijumaa Wikienda, Championi na Spoti Xtra, kisha funua ukurasa wa pili ambapo utakutana na kuponi yenye maelekezo ya namna ya kushiriki.

Itume namba maalum inayoonekana juu ya kuponi hiyo kwa njia ya meseji mwenda namba 0719386533. Hakikisha unaihifadhi kuponi au gazeti lako kwani litahitajika wakati wa kuchukua zawadi.

 

Comments are closed.