The House of Favourite Newspapers

BREAKING NEWS: NDEGE NDOGO YA ABIRIA YAANGUKA MAFIA PWANI

 

NDEGE ndogo ya abiria (5H-NOW) iliyokuwa inatokea Zanzibar-Dar es Salaam  kisha kwenda Mafia imeanguka na kuwaka moto maeneo ya Mafia, ambapo mashuhuda wanasema rubani amefanikiwa kufungua mlango na kuwaokoa abiria.

Watu watano wanadaiwa kujeruhiwa huku watatu hawajulikani walipo katika ajali hiyo.

Kamanda wa Polisi, Kanda Maalumu ya Kibiti, Onesmo Lyanga,  amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na atatoa taarifa zaidi baadaye.

Comments are closed.