The House of Favourite Newspapers

BREAKING NEWS: NECTA YATANGAZA MATOKEO KIDATO CHA SITA, YAPO HAPA

Katibu Mtendaji wa Necta, Dk Charles Msonde

KATIBU Mkuu Baraza la Mitihani la Taifa (Necta) leo akiwa Mjini Zanzibar ametangaza matokeo ya kidato cha sita  kazitaja shule zilizoshika mkia kuwa ni pamoja na ya wasichana ya Jangwani, ya Jijini Dar es Salaam.

 

Ubora wa ufaulu kwa watahiniwa wa shule unaonesha kuwa jumla ya watahiniwa 72,866 sawa na 95.52% wamefaulu katika daraja la kwanza hadi la tatu wakiwemo wasichana 30,619 sawa na 95.92% na wavulana 42,247 sawa na 95.23%. Waliopata daraja la kwanza ni 8,168.

 

Shule 10 zilizofanya vizuri zaidi ni:– 1.Kibaha 2.Kisimiri 3.Kemebos 4.Mzumbe 5.Feza Boys 6.Marian Boys 7.Ahmes 8. St.Marys Mazinde Juu 9.Marian Girls 10.Feza Girls

 

Shule 10 zilizofanya vibaya zaidi ni:- 1.Forest Hill, 2.Jang’ombe, 3.Jangwani, 4. St. James Kilolo, 5.White Lake, 6.Aggrey, 7.Nyailigamba, 8.Musoma Utalii, 9.Ben Bella, 10.Golden Ridge

BONYEZA HAPA KUYATAZAMA

Comments are closed.