The House of Favourite Newspapers

Breaking News: Serikali Kufuta Kodi Taulo za Kike – Video

SERIKALI imesema inapendekeza kuondoa kodi ya ongezeko la thamani (VAT) kwenye taulo za kike nchini ili kuweza kuwapa fursa wanafunzi waliopo mashuleni na vijijini, akina mama na wasichana kuzipata kwa bei nafuu.

 

Akizungumza bungeni leo Juni 14, 2018 wakati alipokuwa anaendelea kusoma Bajeti ya Mwaka wa Fedha 2018/2019, Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango amesema amefanya uamuzi huo kutokana na sheria ya kodi ya ongezeko la thamani kumpa mamlaka ya kufanya hivyo.

 

“Napendekeza kusamehe kodi ya ongezeko la thamani (VAT) kwenye taulo za kike, lengo la hatua hii ni kuwezesha upatikanaji wa bidhaa hiyo adimu kwa bei nafuu ili kuweza kulinda afya ya mama na mtoto wa kike hasa watoto waliopo mashuleni na vijijini, ni matarajio ya serikali watengenezaji wa bidhaa wa taulo za kike wataziuza kwa bei nafuu baada ya kusamehewa kodi hii hatua”, amesema Dkt. Mpango.

Comments are closed.