The House of Favourite Newspapers

BREAKING: RAIA WA MSUMBIJI JELA MAISHA KWA MADAWA YA KULEVYA

Mtuhumiwa Ana Moisie Chissano alipofikishwa katika Mahakama Kuu Kitengo cha Uhujumu Uchumi jijini Dar  es Salaam.

 

MAHAKAMA Kuu Kitengo cha Uhujumu Uchumi jijini Dar  es Salaam, imemhukumu mwanamke, raia  wa Msumbiji, Ana Moisie Chissano,  kifungo cha maisha  baada ya kupatikana na hatia  ya kukutwa na kilogramu 3.03 za dawa za kulevya aina ya cocaine Hydrochloride.

 

Mshtakiwa amefungwa chini  ya kifungu cha sheria cha 15(1)(b) cha sheria namba 5 ya 2015 cha sheria ya kuzuia na kupambana na dawa za kulevya.

 

Hukumu  hiyo imesomwa leo Desemba 12, 2018 na Jaji Lilian  Mashaka baada ya upande wa mashtaka kuthibitisha mashtaka hayo na kuridhika na ushahidi  wa mashahidi sita wa  upande wa mashtaka waliofika mahakamani  hapo kutoa ushahidi wao.

 

Aidha mahakama  imeamuru dawa hizo za kulevya kuteketezwa kwa utaratibu unaostahili.

 

Chanzo stori: Michuzi Blog

Comments are closed.