The House of Favourite Newspapers

MWISHO WA VITA YA MAKUNDI UEFA LEO

MICHUANO ya Ligi ya Mabingwa Ulaya inaendelea tena leo kwa mechi za mwisho za makundi huku timu kadhaa zikihitaji juhudi za ziada ili ziweze kufuzu kwa hatua ya 16 Bora.

 

Baadhi ya timu zitakuwa zikicheza leo bila presha kwa kuwa zimeshafuzu kwa hatua hiyo, lakini nyingine zitakuwa zikitakiwa kufanya juhudi kubwa sana.

 

Ukitazama kwenye makundi yanayocheza leo, Kundi E, lina timu za Ajax, Bayern Munich, Benfica na AEK Athens.

Kundi hili limeshamaliza kazi yake baada ya Bayern Munich mwenye pointi 13 kuwa tayari ameshafuzu na Ajax mwenye pointi 11 naye kufuzu, hivyo vita hapa leo ni mchezo wa Ajax na Bayern wa kuwania uongozi wa kundi hilo.

 

KUNDI F

Katika vita kwenye kundi hili ambalo lina Manchester City, Hoffenheim, Shakhtar Donest na Lyon, huku mbabe ni Manchester City tu ambaye ameshafuzu kwa hatua inayofuata baada ya kufikisha pointi kumi.

Hata hivyo, Lyon naye anaweza kufuzu kama tu atapata sare kwenye mechi yake ya leo dhidi ya Shakhtar.

Lakini kama Lyon watakubali kichapo basi Shakhtar wenyewe watafuzu na Lyon watakwenda kwenye Kombe la Europa.

 

KUNDI G

Kundi hili lina vigogo, Real Madrid, Moscow, Plzen na Roma, likiwa tayari limeshapata wababe wake baada ya Madrid kufuzu pamoja na Lyon.

Tayari limeshajipanga baada ya Madrid kuwa kinara wa kundi akifuatiwa na Roma ambaye ameshajihakikishia nafasi ya pili, hivyo mechi zao la leo hazina uhondo.

 

KUNDI H

Huku kuna Manchester United, Valencia, Young Boys na Juventus, ambapo vigogo wawili Juventus na Manchester United wenyewe wameshafuzu kwa hatua ya 16 Bora.

Hata hivyo, vita ipo kwenye nafasi ambapo kama United watashinda basi watakuwa wamemaliza kama kinara wa kundi lakini ni kama Juventus watapoteza.

Uhakika ni kwamba Valencia watarejea kwenye Kombe lao maarufu la Europa kwenda kupambana na Arsenal na Chelsea.

Comments are closed.