The House of Favourite Newspapers

Brook Amchapa Amir Khan Kwa TKO

0

BONDIA Kell Brook ameshinda pambano lake dhidi ya Amir Khan baada ya mwamuzi kuingilia kati katika raundi ya sita kufuatia Khan kuvurumishiwa makonde mfululizo. Mahasimu hao wa Uingereza, walipambana juzi kwenye ulingo wa Manchester Arena ambapo kabla ya pambano hilo mabondia hao walitoleana vijembe, vitisho, kejeri na matusi.

 

Baada ya kipigo hicho kutoka kwa Brook, 35, bondia Khan amesema kuwa sasa anafikiria kustaafu kucheza ngumi huku Brook naye akisema anafikiria kutundika glovu licha ya kurejea kwenye ubora wake. “Tutawasikiliza wapendwa wetu na kuona,” alisema Brook baada akizungumzia kuhusu

 

Khan, ambaye pia ana miaka 35, alikiri baada ya kipigo hicho cha sita katika maisha yake ya ndondi, kuwa aliteseka kurejea kwenye ubora katika pambano hilo. “Mapambano 40 ni mengi.

 

Kushinda ubingwa wa dunia mara mbili, kwenda Marekani… Nahitaji kukaa chini na familia yangu, lakini inaonekana naelekea mwisho wa ngumi zangu,” alisema.

Leave A Reply