Simanzi na Vilio Mazishi ya Mkuu wa Shule Aliyejinyonga Buchosa – Video

Waombolezaji wakimwaga mchanga kwenye kaburi wakati wa mazishi.

SIMANZI na vilio vilitawala jana wakati wa mazishi ya Mkuu wa Shule ya Sekondari Migukulama iliyopo Kata ya Nyanzenda Halmashauri ya Buchosa wilayani Sengerema., Benedicto Lweikiza (45) aliyefariki kwa kujinyonga akiwa chumbani kwake na kuzikwa kijijini kwao Kasisa wilayani humo.

Ndugu wakiweka mashada kaburini.

Katika msiba huo uliohudhuriwa na mamia ya wananchi, ndugu, marafiki , wanafunzi na walimu wenzake na marehemu uliibua hisia miongoni mwa waombolezaji huku wakieleza kusikitishwa kwao na uamuzi kwa mwalimu huyo kukatisha maisha yake ghafla.

Benedicto Lweikiza enzi za uhai wake.

Akizungumza na Global TV Online mara baada ya mazishi ya mwalimu huyo, Ofisa Elimu wa Sekondari Wilaya ya Sengerema, Benjamin Sperito alisema marehemu alikuwa mchapakazi na akijituma katika kutekeleza majukumu yake ya ualimu hivyo ameacha pengo kubwa katika tasnia hiyo kwani walimtegemea kwa mambo mengi.

Dada wa marehemu akiaga mwili wa kaka yake.

Naye Mhandisi Benard Mtutuzi amabye ni mjomba wa marehemu alieleza namna walivyoshirikiana na Lweikiza katika mambo mbalimbali hasa ya ujenzi wa Taifa huku akieleza kuwa hatomsahahu mwalimu huyo kwa utendaji wake wa kazi mzuri uliotukuka.

 

Bibi wa marehemu akiaga mwili wa mjukuu wake.

Aidha Mtutuzi amewasihi wananchi wengine kutumia busara katika kufanya maamuzi ili yasije yakagharimu maisha yao na jamii inayowazunguka.

Mwili ukipelekwa kaburini.

Aidha watoto wa Marehemu ambao ni Fredy Lweikiza na Frank Lweikiza (14) walieleza namna walivyopokea kwa masikitiko taarifa za kifo cha baba yao.

 

Watoto wa marehemu wakiweka mashada.

“Shangazi alikuwa anapika, alipoivisha akawa amekwenda kumuangalia baba, lakini akakuta ananing’inia dirishani ndipo akaja kuniita, baada ya kuchungulia dirishani nikamuona baba akiwa amekata roho tukamuita Fredy pamoja na majilani na walimu wengine wakawa wamefika”, alisema Frank.

Wanafunzi wakiweka mashahada.

Watoto hao walionekana kuwa wenye simanzi kubwa kwani mama yao nay7e alishafariki miaka mitano iliyopita.

Wanafunzi wakiwa wenye simazni.

Lweikizaalifariki kwa kujinyonga Septemba 9, saa tisa alasiri katika Mtaa wa Kilabela Kata ya Nyatukala wilayani Sengerema mkoani Mwanza.

Walimu wenzake wakiweka mashada.

nn

Walimu wenzake wakiaga.

NA IDD MUMBA | GLOBAL TV, MWANZA.

Simanzi na Vilio Mazishi ya Mkuu wa Shule Aliyejinyonga Buchosa

Loading...

Stori zinazo husiana na ulizosoma

Toa comment