Bunge Kupiga Kura Tena Kumshtaki Trump Leo

Spika Nancy Pelosi.

BUNGE la Marekani litapiga kura kwa mara ya pili kihistoria leo Januari 13, 2021 baada ya Makamu wa Rais Mike Pence kukataa kuyatumia Marekebisho ya 25 ya Katiba ya Marekani na kumwondoa Rais (Donald Trump) licha ya chama cha Democrats kumtaka achukue hatua hiyo.

Pence alikataa kufanya hivyo baada ya kutuma barua kwenda kwa Spika, Nancy Pelosi, jana akisema hatafanya aliyotakiwa.

 

Katika kura iliyopigwa jana usiku saa 5:30, Bunge lilipiga kura 223 kwa 205 kupitisha azimio hilo ambalo halimlazimisha rais kuachia ngazi.

 

Wabunge wa chama cha Democratic, watajaribu leo (Jumatano) kumshtaki Trump kwa mara ya pili kutokana na kuhusika kwake  katika mashambulizi yaliyofanyika Bunge (Capitol).

Makamu wa Rais, Mike.

Toa comment