The House of Favourite Newspapers

BUSHOKE KUMFANYIA SAPRAIZ NYOSH EL SADAAT DAR LIVE

Image result for BUSHOKE

PATAKUWA hapatoshi! Wakati mashabiki wengi wa Muziki wa Dansi wakiwa tayari kusubiri utambulisho wa Bendi ya Bogos, msanii wa Muziki wa Bongo Fleva, Ruta Maxi Bushoke ‘Bushoke’ amethib-itisha kufanya bonge la sapraiz katika utambulisho huo unaotarajia kufanyika Oktoba 6, mwaka huu ndani ya Uwanja wa Taifa wa Burudani, Dar Live uliopo Mbagala-Zakhem jijini Dar.

 

Akizung-umza na Showbiz Xtra, Meneja na Mratibu wa Dar Live, Rajabu Mteta ‘KP Mjomba’ alisema, usiku huo utatambulika kama Usiku wa Mwafrika ambao utafanyika utambulisho baab’kubwa wa Bendi ya Bogos chini ya Nyoshi el Sadaat.

 

“Kwa wale wana Temeke hii ni kwa ajili yenu kabisaa! Kwa kiingilo cha shilingi 5,000 tu utapata kushuhudia bonge moja la shoo kutoka kwa Bendi ya Bogos ambayo usiku huo itatambulishwa rasmi kwa wakazi wa Temeke tangu kuanzishwa kwake.

 

Mashabiki watapata kusikia vibao kibao kutoka kwa Nyoshi kikiwemo Naliamsha Dude huku Bushoke akipanda kwa mara ya kwanza tangu kuwa kwake kimya kwa muda mrefu,” alisema KP Mjomba.

Shoo hiyo imeandaliwa kwa udhamini wa DJ Tassy kwa kushirikiana na Nambiza Entertainment na Dar Live.

Comments are closed.