The House of Favourite Newspapers

BUSUNGU: LIPULI MSINITAFUTE NIPO DOM NAFANYA BIASHARA

HIVI karibuni Kocha wa Lipuli FC, Selemani Matola aliweka wazi kuwa hajui alipo mchezaji wake Malimu Busungu na kwamba kambini hakuwepo lakini Championi limemnasa mchezaji huyo ambaye amesema wazi kuwa ameachana na soka rasmi.

 

Busungu ambaye alisajiliwa na Lipuli msimu uliopita akitokea Yanga, amekuwa na mgogoro na viongozi wake hao kwa madai ya kutolipwa stahiki zake.

 

Akizungumza na Championi Jumamosi moja kwa moja kutoka Dodoma, Busungu alisema kwa sasa hana mpango wa kurejea kwenye soka baada ya kushindwa kuelewana na viongozi wake hasa kwa upande wa malipo.

 

“Kwa sasa sifikirii kujiunga na timu yoyote ili kuendelea na mpira licha ya kuwa na kipaji itakuwa ni nafasi kwangu kuweza kufanya biashara ili kuendeleza maisha yangu pamoja na familia ila siyo mpira kwa sasa.

 

“Nataka amani ndani ya moyo ndiyo maana nimeamua kuachana na soka, hivyo wakati wangu ni sasa kutafuta mafanikio kupitia upande mwingine, kwa sasa nipo Dodoma nafuatilia masula ya masoko kabla sijaanza kufanya biashara, kwa hiyo wasinitafute,” alisema Busungu.

Lunyamadzo Mlyuka, Dar es Salaam

LIVE: Mtoto wa Dudu Baya amzungumzia Baba Yake

Comments are closed.