The House of Favourite Newspapers

BUSUNGU: Njombe Mji Niacheni, Nasaini Ndanda FC

0
Malimi Busungu.

STRAIKA Malimi Busungu yupo katika hatua ya mwisho ya kujiunga na Ndanda FC ya Mtwara ili akaiongezee nguvu kwenye safu yao ya ushambuliaji.

 

Busungu ambaye msimu uliopita aliichezea Yanga, pia alikuwa akitakiwa na timu ya Njombe Mji ya mkoani Njombe lakini hawakufikia muafaka, hivyo sasa amekubaliana na Ndanda na muda wowote atajiunga nayo.

 

Busungu amesema licha ya kuwa kwenye hatua za mwisho kumalizana na Ndanda, viongozi wa Njombe Mji wamekuwa wakimsumbua wakitaka kumsajili lakini yeye ameamua kuachana nao kwani aliona kama hawakuwa siriaz.

 

“Njombe Mji walinitaka na tukafanya nao mazungumzo lakini baada ya muda walikaa kimya nikaona hawana nia na mimi ndipo nikaamua kufanya mazungumzo na Ndanda na tumekubaliana kila kitu, nawashangaa Njombe Mji hivi sasa wanaanza tena kunisumbua wakiitaka saini yangu,” alisema Busungu.

 

Sweetbert Lukonge | CHAMPIONI JUMATATU| Dar es Salaam

Leave A Reply