The House of Favourite Newspapers

CAG Akabidhi Ripoti kwa Rais Magufuli, Aanika Mdudu – Video

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Magufuli, leo Machi 27, 2018, anapokea ripoti kutoka kwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali, Profesa Musa Assad.

 

Tukio hilo limefanyika Ikulu jijini Dar es Salaam na kluhudhuriwa na viongozi mbalimbali akiwemo Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama, Meja Jen. Venance mabeyo, Naibu Spika wa Bunge Dkt. Tulia Ackson, Mwenyekiti wa Kamati ya Hesabu za Serikali za Mitaa, Jaji Mkuu, Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi, IGP Simon Sirro na wengine.

 

Akizungumza wakati wa kukabidhi ripoti hiyo kwa Rais Magufuli, Profesa Musa Assad amesema;

“Matibabu ya nje ya nchi kwa mwaka wa fedha 2017-2018 yamefikia kiasi cha Shilingi Bilioni 46. Tumebaini kuna taasisi nane zimefanya manunuzi ya vifaa kazi na huduma yenye thamani ya bilioni Tsh. 53, vilivyoagizwa na kulipiwa lakini havikupokelewa.

 

“Pia, kuna malipo yanayofikia Dola za Marekani 161,382 yamefanyika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam bila mkataba katika pande zote mbili. Zipo fedha za ushuru wa mafuta na usafirishaji ambazo zimekusanywa na TRA zinafikia bilioni 15, lakini nazo hazikupelekwa katika Mfuko wa Barabara (ROAD FUND).”

Mbali na hayo, Profesa Assad ameeleza kuwa kuna deni la Taifa limeongezeka kutoka trilioni 41 hadi trilioni 46 kwa mwaka kipindi cha mwaka mmoja.

VIDEO: FUATILIA HAPA

Comments are closed.