The House of Favourite Newspapers

Carlinhos, Job Kamili Kuivaa Simba

0

KIUNGO wa Yanga, Carlos Carlinhos na beki wa timu hiyo, Dickson Job, huenda wakaanza kwenye mchezo dhidi ya Simba ikiwa Kocha Mkuu, Nasreddine Nabi atawapanga kutokana na sasa kuwa fiti.

 

Carlinhos alipata maumivu kwenye mchezo wa Kombe la Shirikisho dhidi ya Tanzania Prisons uliochezwa hivi karibuni, huku Job akiwa anasumbuliwa na tatizo la nyama za paja lililomuweka nje kwa siku kadhaa.

 

Habari kutoka ndani ya Yanga, zimeeleza kuwa tayari nyota hao wameanza mazoezi na ikimependeza kocha, wataivaa Simba Jumamosi ijayo kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar.

 

“Carlinhos yupo fiti kwa sasa pia Job naye anaendelea vizuri, hivyo kwa sasa ni kazi ya mwalimu kuwaandaa wachezaji wake katika mechi zijazo,” ilieleza taarifa hiyo.

 

Ofisa Habari wa Yanga, Hassan Bumbuli aliliambia Spoti Xtra kuwa wachezaji wao wapo vizuri na wameanza maandalizi kwa ajili ya mechi zijazo ikiwemo dhidi ya Simba.

 

Katika kikosi cha Yanga hivi sasa, majeruhi wa muda mrefu, Mapinduzi Balama na Yassin Mustapha ambaye bado hajawa fiti, huenda wakaukosa mchezo huo ambao unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa

STORI: LUNYAMADZO MLYUKA

Leave A Reply