The House of Favourite Newspapers

CHADEMA: “CCM Wanamtumia LOWASSA, Hatutakubali” – VIDEO

WANACHAMA wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) wamekilalamikia Chama Cha Mapinduzi (CCM) wakidai kuwa chama hicho kinalitumia jina la mjumbe wao, Edward Lowassa, katika kampeni zao za uchaguzi kama njia ya kuwavuta wananchi waje kuwasikiliza.

 

Wakizungumza na wanahabari jana, Mwenyekiti wa Baraza la Vijana Chadema (Bavicha), Patrick Ole Sosopi na mgombea wa ubunge katika Jimbo la Monduli, Yonas Masiaya, wamesema CCM imeishiwa Sera na nguvu ya kufanya kampeni hivyo wameanza kuwadanganya wananchi kuwa Lowassa anataka kurudi CCM hivyo wakusanyike kwenye mikutano yao ya kampeni jambo ambalo sio kweli.

VIDEO: FUTAILIA MKUTANO HUO HAPA

Comments are closed.